Swali: Jana imamu wa msikiti moja kwa moja baada ya ´Aswr alitangaza kwamba khabari zimethibitishwa kuwa jua lipatajwa na kwamba wataswali swalah ya kupatwa kwa jua 16.30 na kuwataka watu wahudhurie. Je, hili ni jambo lililowekwa katika Shari´ah?

Jibu: Swalah ya kupatwa kwa jua haiwajibiki isipokuwa pale itapoonekana kuwa jua limepatwa. Hakuzingatiwi khabari au maneno ya wataalumu wa nyota. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Jua na mwezi ni alama mbili miongoni mwa alama za Allaah. Havipatwi kwa kufariki au kupata uhai kwa yeyote. Allaah kwavyo anawatia khofu waja Wake. Mkiona kitu katika hayo basi kimbilieni kumtaja, kumuomba, kumtaka msamaha, kutoa swadaqah, kuwaachia watumwa huru na kuswali misikitini mpaka iondoke hali hiyo.”[1]

Haijuzu kutangaza jambo hili mpaka kuonekane kua jua limepatwa. Pindi itapoonekana hali hiyo ndio watu watatangaziwa:

الصلاة جامعة

“Hii ni swalah ya pamoja.”

Hapo ndipo watu wataenda na kuswali.

[1] Muslim (911).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (16)
  • Imechapishwa: 28/04/2021