Kuthibitisha dhati kunalazimisha kuthibitisha sifa

Swali: Je, tunaweza kusema ya kwamba yule mwenye kuthibitisha Dhati [ya Allaah] amethibitisha vilevile Sifa na kwamba mwenye kuthibitisha Sifa amethibitisha Dhati?

Jibu: Mwenye kuthibitisha Dhati analazimika kuthibitisha Sifa. Hili linamlazimu. Kuna uwezekano vilevile asizithibitishe kama Jahmiyyah. Lakini hili kwa hali yoyote linamlazimu. Kwa kuwa hakuna dhati ilio kivyake isiyokuwa na sifa. Kitu kisichokuwa na sifa ni kitu kisichopatikana. Hivyo, kuthibitisha Dhati kunalazimisha kuthibitisha Sifa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (05) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_05.mp3
  • Imechapishwa: 31/05/2015