Kutazama nywele za mwanamke mposwaji

Swali: Je, inafaa kutazama nywele?

Jibu: Kilichotangaa kwa wanazuoni ni kutazama uso na mikono. Wengine wamesema kuwa mtu atazame vile viungo ambavyo mara nyingi huonekana. Hapana vibaya ikiwa ataona nywele, kwa sababu ni kitu ambacho mara nyingi huonekana nyumbani kwake na kinamvutia pia. Nywele nzuri humvutia pia. Kwa mujibu wa maoni ya sawa ni kwamba hapana vibaya akamtazama uso wake, mikono yake, miguu yake na nywele zake.  Kwa sababu nywele huonekana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23829/هل-يجوز-النظر-الى-شعر-المخطوبة
  • Imechapishwa: 07/05/2024