Swali: Je, kutawadha kwa kila swalah ni Sunnah maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au ni kwake na kwa yeyote atakayependa?

Jibu: Ni Sunnah kwa wote. Atawadhe kwa ajili ya Dhuhr wudhuu´ wake, kwa ajili ya ´Aswr wudhuu´ wake. Ikiwa bado yuko na twahara, basi kutawadha tena ni bora zaidi. Akiacha na akaswali kwa twahara ya kwanza pia haina neno. Akitawadha kwa ajili ya ´Aswr na akaswali kwa hiyohiyo Maghrib, kisha akatawadha kwa ajili ya Maghrib na akaswali kwa hiyohiyo ´Ishaa, hakuna tatizo na hakuna dhambi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya ufunguzi wa mji wa Makkah aliswali swalah kadhaa kwa wudhuu´ mmoja ili kuwaonesha watu kwamba hakuna tatizo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31704/ما-حكم-الوضوء-لكل-صلاة
  • Imechapishwa: 16/11/2025