Kutanguliza mbele akili kabla ya dalili – alama ya Ahl-ul-Bid´ah

Swali: Tunawaona vijana wengi wanatanguliza mbele akili kabla ya andiko na hawakinaiki isipokuwa kwa akili yao na wanajifanya kujahili umuhimu wa andiko. Tunaomba nasaha juu ya hilo?

Jibu: Hii ni alama ya wapotevu ambao wanatanguliza mbele akili kabla ya andiko. Kwa msemo mwingine wanatanguliza mbele fikira na akili zao kabla ya Qur-aan na Sunnah. Akili ni fupi. Lakini andiko la Qur-aan na Sunnah ni zenye kukamilika na ni za kweli. Haziingiliwi na shaka. Muislamu anatanguliza mbele Qur-aan na Sunnah na hatangulizi mbele akili na fikira mbele ya Qur-aan na Sunnah:

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا

“Haiwi kwa muumini mwanamme na wala kwa muumini mwanamke pindi Allaah anapohukumu na Mtume Wake jambo lolote iwe wana khiyari katika jambo lao – na yule anayemuasi Allaah na Mtume Wake, basi kwa hakika amepotoka upotofu wa wazi.”[1]

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا

”Kile alichokupeni Mtume basi kichukueni na kile alichokukatazeni basi kiacheni.”[2]

Huu ndio wajibu; unapaswa kuamini Qur-aan na Sunnah na utangulize mbele Qur-aan na Sunnah kabla ya kila fikira, akili, maoni na kila mtazamo miongoni mitazamo. Unapaswa kutanguliza mbele Qur-aan na Sunnah.

[1] 33:36

[2] 59:07

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (01)
  • Imechapishwa: 13/02/2024