Kutahadharisha ufisadi wa aliyetangulia mbele ya haki

Swali: Ikiwa kuna mtu aliyekufa akiwa na ufisadi mwingi. Je, inafaa kuwatahadharisha wenzake waliobaki kutokana na matendo yake?

Jibu: Hakuna tatizo ikiwa ufisadi wake ulikuwa dhahiri na maasi yake yalikuwa wazi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati kulipopitishwa jeneza na Maswahabah wakamweleza kwa shari, naye akasema:

”Imewajibika.”

Hakuwakataza kufanya hivyo. Hili linafasiriwa kwa maana kwamba maasi ya mtu huyo yalikuwa dhahiri. Mtu ambaye maasi yake ni ya wazi hakuna usengenyi. Hakuna juu yake usengenyi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25245/هل-يجوز-تذكير-الناس-بفساد-من-مات
  • Imechapishwa: 20/02/2025