Swali: Baadhi ya Suufiyyah wanasema kuwa nyimbo za sifa zinazoimbwa katika vikao vya mirungi na harusi ni katika kumtaja Allaah. Je, haya ni sahihi?
Jibu: Suufiyyah, kama alivosema Ibn Hazm katika “al-Faswl”:
“Allaah ameupa mtihani Uislamu kwa Suufiyyah na Shiy´ah.”
Suufiyyah na Shiy´ah ni wenye kuwatengenezea njia wakomunisti. Ni watu wenye kutegemea maoni, ndoto na kufunua yaliyofichwa, na hawalazimiani na Qur-aan na Sunnah. Kama alivosema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, huenda mbali zaidi mpaka Ibn ´Arabiy akasema:
Mola ni mja na mja ni Mola
Laiti ningelijua ni nani ´ibaadah zinamuwajibikia
Wendawazimu wa Suufiyyah hauna mwisho. Lakini Suufiyyah wa zamani walikuwa wanaweza kujiliwa na hali fulani ya usingizi kwa sababu ya upweke na njaa. Suufiyyah leo wanajiliwa na hali ya usingizi kwa sababu ya dunia. Wamepewa mtihani wa dunia. Wanatafuna mirungi, wanavuta sigara na kuwalaghai watu pesa zao. Hawajali hata kama mtu atawaita katika ukafiri. Hawajali hata kama mtu atatetea ukafiri. Baadhi ya Suufiyyah wamesema kuwa ni bora kuwa mwizi katika upweke kuliko kupea mtihani wa dunia. Katika “Swifat-us-Swafwah” cha Ibn-ul-Jawziy imekuja ya kwamba Imaam ash-Shaafi´iy amesema kuwa endapo mtu atapambazuka akiwa Suufiy basi itafika jioni akiwa mpumbavu
Adhkaar na nyimbo za sifa zinazotajwa katika mawaidha ndani yake kuna Bid´ah, Bid´ah kwa njia za Tawassul na shirki. Baada ya hapo wanakaa kwa ajili ya kutafuna mirungi. Hamu yao kubwa ni kuwavuta watu kwao. Isitoshe nina kanda kuhusu Suufiyyah.
Mabwanyenye wa Suufiyyah kama vile Ibn Sab´iyn, at-Tilmisaaniy, al-Hallaaj na Ibn ´Arabiy wamefikia kuishilia kupinga Shari´ah na kuhalalisha mambo ya haramu. Baadhi yao wamesema kuwa Fir´awn alikuwa bora kuliko Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam); Fir´awn alikuwa mpwekeshaji na Muusa alikuwa mshirikina. Haya yametajwa na Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) katika mjeledi wa pili katika “Majmuu´-ul-Fataawaa”. Wanasema kuwa Fir´awn hakuridhia aabudiwe Allaah peke yake kwa sababu kila kilichoko katika ulimwengu ni Allaah, ilihali Muusa alikuwa mshirikina kwa sababu alitaka Allaah pekee ndiye aabudiwe. Napendekeza kwa ndugu wasome mjeledi wa pili wa “´Majmuu´-ul-Fataawaa” wa -ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) waone wendawazimu wao.
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 325-326
- Imechapishwa: 04/06/2025

Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 325-326
Imechapishwa: 04/06/2025
https://firqatunnajia.com/kutafuna-mirungi-na-kulala/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket