Kuswali Raatibah ya Fajr kila siku baada ya Fajr

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kuswali Raatibah ya al-Fajr daima baada ya Swalah?

Jibu: Haijuzu kufanya hivi. Hili linakuwa kwa yule iliyempita pasina khiyari yake. Kwa mfano hakuamka isipokuwa baada ya kukimiwa Swalah, huyu ataiswali baada ya Swalah. Ama mtu kukusudia hili, haijuzu. Kwa kuwa huu ni wakati wa makatazo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (06) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-8-5.mp3
  • Imechapishwa: 10/11/2014