Swali: Kipindi cha mwisho tumepewa mtihani wa baadhi ya maimamu wa misikiti ambao wanakhafifisha swalah ukhafifisha kwa njia ya kwamba imamu anarukuu kabla ya mswaliji kumaliza kusoma al-Faatihah, imamu anarukuu baada ya Tashahhud ya mwisho kabla ya mswaliji kumaliza kusoma Tashahhud hiyo na huenda wakati mwingine akatoa salamu kabla ya mswaliji kumaliza kuomba ulinzi dhidi ya mambo mane yanayotambulika. Ni ipi hukumu kwa upande wa imamu na maamuma?
Jibu: Kwa upande wa imamu ni haramu kwake kufanya hivo. Wanachuoni wamesema kuwa ni haramu kwa imamu kuharakisha uharakisho utakaowafanya waswaliji kukosa kufanya yale yanayowawajibikia. Ni wajibu kwa imamu kuwaongoza watu kwa mfano wa vile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyokuwa akiwaongoza Maswahabah wake na awape watu nafasi. Lakini baadhi ya maimamu wakiona watu wanamkubali kwa vile anavyokhafifisha swalah au anatanguliza Iqaamah anadanganyika na hilo. Hilo halimfai kitu mbele ya Allaah siku ya Qiyaamah. Wajibu kwake ni kutekeleza amana na awaswalishe watu kama ambavo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyokuwa akiwaswalisha Maswahabah wake.
Kuhusiana na maimamu, ikiwa hawawezi kutekeleza yale mambo ya wajibu, basi ni wajibu kwao kuswali katika misikiti mingine ambayo wataweza kutekeleza yale mambo ya wajibu. Si halali kwao kuwa nyuma ya imamu huyu ambaye hawawezi kutekeleza mambo ya wajibu. Wakiweza kuirekodi swalah kisha wakawapelekea wasimamizi wa idara ya msikiti ili ima waweze kumbadilisha au kumrekebisha basi itakuwa ni jambo la kheri.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (48) http://binothaimeen.net/content/1106
- Imechapishwa: 09/04/2019
Swali: Kipindi cha mwisho tumepewa mtihani wa baadhi ya maimamu wa misikiti ambao wanakhafifisha swalah ukhafifisha kwa njia ya kwamba imamu anarukuu kabla ya mswaliji kumaliza kusoma al-Faatihah, imamu anarukuu baada ya Tashahhud ya mwisho kabla ya mswaliji kumaliza kusoma Tashahhud hiyo na huenda wakati mwingine akatoa salamu kabla ya mswaliji kumaliza kuomba ulinzi dhidi ya mambo mane yanayotambulika. Ni ipi hukumu kwa upande wa imamu na maamuma?
Jibu: Kwa upande wa imamu ni haramu kwake kufanya hivo. Wanachuoni wamesema kuwa ni haramu kwa imamu kuharakisha uharakisho utakaowafanya waswaliji kukosa kufanya yale yanayowawajibikia. Ni wajibu kwa imamu kuwaongoza watu kwa mfano wa vile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyokuwa akiwaongoza Maswahabah wake na awape watu nafasi. Lakini baadhi ya maimamu wakiona watu wanamkubali kwa vile anavyokhafifisha swalah au anatanguliza Iqaamah anadanganyika na hilo. Hilo halimfai kitu mbele ya Allaah siku ya Qiyaamah. Wajibu kwake ni kutekeleza amana na awaswalishe watu kama ambavo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyokuwa akiwaswalisha Maswahabah wake.
Kuhusiana na maimamu, ikiwa hawawezi kutekeleza yale mambo ya wajibu, basi ni wajibu kwao kuswali katika misikiti mingine ambayo wataweza kutekeleza yale mambo ya wajibu. Si halali kwao kuwa nyuma ya imamu huyu ambaye hawawezi kutekeleza mambo ya wajibu. Wakiweza kuirekodi swalah kisha wakawapelekea wasimamizi wa idara ya msikiti ili ima waweze kumbadilisha au kumrekebisha basi itakuwa ni jambo la kheri.
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (48) http://binothaimeen.net/content/1106
Imechapishwa: 09/04/2019
https://firqatunnajia.com/kuswali-nyuma-ya-imamu-anayeharakisha-swalah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)