Swali: Wapo baadhi ya ndugu wanaowakimbiza watu kuswali katika msikiti wa Ibn ´Abbaas huko Twaaif na wakisema kuwa umejengwa juu ya makaburi. Nini maoni yenu?
Jibu: Hili ni makosa na ni ujinga. Mara makaburi yanapofukuliwa kwa manufaa ya waislamu, inajuzu kuswali mahali hapo. Hapana vibaya kuswali katika msikiti wa Ibn ´Abbaas kwa sababu makaburi yalifukuliwa kwa ajili ya manufaa ya waislamu. Kwa hiyo hapana kizuizi juu ya hilo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alijenga msikiti wake katika mahali palipokuwa na makaburi. Msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ulikuwa na makaburi, akaamrisha yafukuliwe na yaondolewe. Pia ulikuwa na mashimo na magofu, akaondoa. Vilevile ulikuwa na mitende, ikakatwa, kisha ukajengwa msikiti. Makusudio ni kwamba mara makaburi yanapohamishwa kwa manufaa, basi hapana vibaya.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30092/ما-حكم-الصلاة-في-مسجد-ابن-عباس-بالطاىف
- Imechapishwa: 07/09/2025
Swali: Wapo baadhi ya ndugu wanaowakimbiza watu kuswali katika msikiti wa Ibn ´Abbaas huko Twaaif na wakisema kuwa umejengwa juu ya makaburi. Nini maoni yenu?
Jibu: Hili ni makosa na ni ujinga. Mara makaburi yanapofukuliwa kwa manufaa ya waislamu, inajuzu kuswali mahali hapo. Hapana vibaya kuswali katika msikiti wa Ibn ´Abbaas kwa sababu makaburi yalifukuliwa kwa ajili ya manufaa ya waislamu. Kwa hiyo hapana kizuizi juu ya hilo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alijenga msikiti wake katika mahali palipokuwa na makaburi. Msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ulikuwa na makaburi, akaamrisha yafukuliwe na yaondolewe. Pia ulikuwa na mashimo na magofu, akaondoa. Vilevile ulikuwa na mitende, ikakatwa, kisha ukajengwa msikiti. Makusudio ni kwamba mara makaburi yanapohamishwa kwa manufaa, basi hapana vibaya.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30092/ما-حكم-الصلاة-في-مسجد-ابن-عباس-بالطاىف
Imechapishwa: 07/09/2025
https://firqatunnajia.com/kuswali-ndani-ya-msikiti-ambao-kumefukuliwa-makaburi/