Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali na pesa mfukoni, kitambulisho au vitu vingine vilivyo na picha? Ikiwa inajuzu ni jambo limependekezwa kuvitenga mbali wakati wa kuswali?

Jibu: Ukiviweka mfukoni mwako na ukavificha ni sawa kutokana na dharurah. Ikiwa unataka kuweka pesa kwenye mlango wa Msikiti pamoja na viatu vyako mpaka wakati utapomaliza, hii ni khiyari yako. Lakini ujue kuwa zitachukuliwa! Haitakikani mtu kuwa na upetukaji mipaka wa namna hii. Hii ni dharurah inayofanywa na mtu wakati wa haja. Lakini pamoja na hivyo azifiche [mfukoni].

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_01.mp3
  • Imechapishwa: 03/07/2018