Swali: Ni sahihi kutumia dalili kwamba ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) damu ilikuwa ikimtoka na hakutawadha?

Jibu: Ndio, hii ni dalili inayotumiwa na wale wanaosema kuwa damu nyingi haitengui wudhuu´, kwa kuwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) aliendelea na swalah yake. Vilevile Maswahabah walikuwa wakipatwa na mikuki na wakitokwa na damu wakati wamesimama na kuswali. Pamoja na hivyo wanaendelea kuswali. Hii ni dalili inayotumiwa na wale wanaoonelea kuwa damu haitengui wudhuu´ hata kama ni nyingi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (5) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–01041434.mp3
  • Imechapishwa: 21/10/2016