Swali: Baadhi ya ndugu wanawakataza watu kuswali katika msikiti wa Ibn ´Abbaas Twaa´if na wanasema kuwa ni msikiti uliojengwa juu ya makaburi. Unasemaje?

Jibu: Hili ni kosa. Pindi makaburi yatakapochimbuliwa kwa ajili ya manufaa ya waislamu basi itafaa kuswali maeneo hapo. Kwa ajili hiyo ni sawa kuswali katika msikiti wa Ibn ´Abbaas. Kwa sababu ni makaburi yaliyochimbuliwa kutokana na manufaa ya waislamu. Hivyo hakuna neno kufanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) msikiti wake ulijengwa maeneo kulipo makaburi. Msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kulikuweko makaburi. Ndipo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaamrisha kuyachimbua na kuyaondosha. Pia kulikuweko mashimo ambayo yaliondoshwa. Kadhalika kulikuweko mitende ikakatwa. Baada ya hapo ndipo kukajengwa msikiti. Tunachotaka kusema ni kwamba pindi makaburi yatakapochimbuliwa kutokana na manufaa kutakuwa hakuna neno [kuswali maeneo hapo].

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3985/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D8%A8%D9%85%D8%B3%D8%AC%D8%AF-%D9%81%D9%8A-%D9%85%D9%88%D8%B6%D8%B9-%D9%82%D8%A8%D9%88%D8%B1-%D8%AA%D9%85-%D9%86%D8%A8%D8%B4%D9%87%D8%A7
  • Imechapishwa: 31/10/2020