Swali: Mtu anaweza kuchukua kutoka kwenye kichwa cha khabari “Kusichinjwe sehemu ambapo kunachinjwa kwa ajili ya mwengine asiyekuwa Allaah” ya kwamba haifai kuswali kwenye misikiti ya Ahl-ul-Bida´ah?

Jibu: Bid´ah zinatofautiana. Ikiwa ni Bid´ah za kikafiri na msikiti huu unafanya Bid´ah za kikafiri na za shirki, kusiswaliwe ndani yake. Ama ikiwa Bid´ah iko chini ya kufuru na shirki, ni maasi. Kwa hivyo usiache kuswali pamoja nao. Swali pamoja nao swalah ya mkusanyiko.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (33) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majid-10-11-1436-01.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017