Kuswali kwa kuzielekea hita za moto

Swali: Kumejitokeza makinzano msikitini kuhusiana na hita za umeme mbele ya waswaliji na kama ni haramu au inachukiza kuswali kwa kuzielekea? Je, ni haramu au inachukiza kuswali kwa kuuelekea moto?

Jibu: Baadhi ya wanazuoni wamechukizwa na kuswali kwa kuuelekea moto na wengine hawakufanya hivo. Wale wenye kuona kuwa inachukiza wametoa sababu kwamba ni kujifananisha na waabudia moto. Ni jambo linalotambulika kuwa waabudia moto huabudu moto uwakao. Kwa msemo mwingine haichukizi kuswali kwa kuelekea moto usiowaka. Jengine ni kwamba watu wanahitaji hita hizi wakati wa majira ya baridi ili kukota moto. Wakiziweka hita hizo kwa nyuma yanaondoka yale manufaa yake au wakiziweka upande wa kulia au wa kushoto hawatonufaika nazo isipokuwa kidogo. Kanuni inayotambulika kwa wanazuoni ni kwamba haja inajuzisha kilichochukizwa. Isitoshe mara nyingi ni kwamba hita hizi haziwi mbele ya imamu, bali zinakuwa mbele ya maamuma, jambo ambalo linawepesisha jambo lake. Kwa sababu imamu ndiye kiigiezo, na kwa ajili hiyo ikawa ile Sutrah yake ndio Sutrah ya maamuma – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

1409-06-22

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/409)
  • Imechapishwa: 03/04/2026