Swali: Ni ipi hukumu ya kususia bidhaa za baadhi ya nchi zinazowaunga mkono mayahudi kwa ajili ya kusimama pamoja na ndugu zetu waislamu huko Palestina?

Jibu: Kususia ni jambo zuri. Nimesikia kwamba kuna fatwa ya Shaykh ´Abdullaah bin Jibriyn kuhusu jambo hili. Basi tunamuomba Allaah awape ushindi Mujaahiduun na awadhalilishe makafiri. Tunamuomba Allaah awape ushindi ndugu zetu Mujaahiduun huko Palestina, Chechenia na Kashmiyr. Tunamuomba Allaah awahurumie kwa udhaifu wao, awarekebishie yaliyowafika, aunganishe safu zao, aunganishe kauli yao. Aidha tunamuomba Allaah aweke khofu katika nyoyo za maadui zao, awadhalilishe, awatawanyishe na awatenganishe vipande vipande na awajaalie kuwa ngawira kwa waislamu. Hakika Yeye ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
  • Imechapishwa: 18/09/2026