Kusoma Suurah yenye Sujuud katika swalah za kusoma kimyakimya

Swali: Kusoma as-Sajdah katika swalah za kusoma kimyakimya?

Jibu: Akiisoma asisujudu ili asiwashawishi watu.

Swali: Kuna imamu anasema kuwa aliisoma na ndani yake kuna Sujuud na alipofika maeneo pa Sujuud akanyanyua sauti kidogo kwenye kipaza sauti halafu wakasikia na wakasujudu baada yake

Jibu: Hakuwa anasujudu ndani yake katika swalah za kusoma kimyakimya. Sunnah ni yeye asiisome. Na akiisoma asisujudu ili asiwatie uzito watu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23743/حكم-قراءة-الامام-اية-سجدة-في-صلاة-سرية
  • Imechapishwa: 19/04/2024