Kusoma Qur-aan kwa pamoja baada ya swalah za faradhi

Swali: Katika ada yetu sisi watu wa Marocco tunasoma Qur-aan kwa pamoja asubuhi na jioni baada ya swalah ya asubuhi na maghrib. Kuna wanaosema kuwa ni Bid´ah.

Jibu: Kulazimiana na kusoma Qur-aan kwa pamoja kwa sauti ya pamoja baada ya kila swalah ya asubuhi na maghrib au nyinginezo ni Bid´ah. Hali kadhalika kulazimiana na kuomba du´aa za pamoja baada ya swalah. Ama kila mmoja akisoma kivyake au wakafundishana Qur-aan kwa njia ya kwamba kila anapomaliza mmoja mwingine na yeye anasoma na wakamsikiliza, hii ni aina bora ya ´ibaadah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Hawatokusanyika watu katika Nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah, wakisoma Kitabu cha Allaah na wakidurusishana nacho isipokuwa huteremkiwa na utulivu, hufunikwa na rahmah, Malaika huwazungumza na Allaah anawataja kwa wale walio Kwake.”

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/342)
  • Imechapishwa: 23/08/2020