Swali: Unasemaje juu ya mtu ambaye anamwigiliza al-Muhaysiniy, as-Sudays au msomaji mwingine wa Qur-aan na analia ile sehemu waliolia wasomaji hawa?

Jibu: Sijui ubaya wowote wa kitendo hichi, ingawa nilisoma kutoka kwa baadhi ya watu wa zama hizi kwamba haijuzu. Anayesema kuwa ni haramu basi alete dalili. Ikiwa ni kulia kutoka kwa nafsi yake, ni sawa. Na ikiwa ni kulia kwa unafiki, haijuzu. Na ikiwa anajilazimisha kulia kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall), hapana vibaya kufanya hivo.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 425-426
  • Imechapishwa: 18/07/2025