Kusoma kwa sauti na kuitikia Aamiyn kwa anayeswali peke yake

Swali: Anaposwali mtu swalah ya ´ishaa peke yake asome kwa sauti yake katika kisomo chake na aitikie “Aamiyn” peke yake?

Jibu: Ndio, ni Sunnah kufanya hivyo, sawa ikiwa anasali peke yake au anaswali pamoja na mkusanyiko. Asome kwa sauti katika swalah za kusoma kwa sauti kama mfano wa swalah ya fajr, ´ishaa na maghrib na aitikie “Aamiyn” kwa sauti. Na akisoma kwa sauti ya chini swalah yake inasihi. Lakini Sunnah ni kusoma kwa sauti.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/96/%D8%AC%D9%87%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%86%D9%81%D8%B1%D8%AF-%D8%A8%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%AA%D9%87
  • Imechapishwa: 07/06/2020