Kusoma al-Faatihah baada ya Rukuu´ ya kwanza ya swalah ya kupatwa kwa jua

Swali: Je, kuna dalili juu ya kusoma tena al-Faatihah katika Rak´ah ya pili katika swalah ya kupatwa kwa jua?

Jibu: Kwa sababu ni Rak´ah. Rak´ah ya pili inazingatiwa kuwa ni yenye kujitegemea na hivyo mswaliji anasoma al-Faatihah. Anaposoma na akarukuu, kisha akainuka inakuwa ni kama Rak´ah ya pili. Kwa ajili hiyo mswaliji asome al-Faatihah na asome Suurah nyingine baada yake. Hivo ndivo wanavoona wanazuoni.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23885/حكم-قراءة-الفاتحة-بعد-الركوع-الثاني-للكسوف
  • Imechapishwa: 25/05/2024