Swali: Je, wakati wa kuchinja tunatakiwa kusema:
قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ
”Sema: “Hakika swalah yangu na kichinjwa changu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah pekee, Mola wa walimwengu.”[1]
Jibu: Wakati wa kuchinja kawaida mtu anasema:
باسم الله
“Kwa jina la Allaah.”
Kuhusu kusema:
قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ
”Sema: “Hakika swalah yangu na kichinjwa changu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah pekee, Mola wa walimwengu.”
hayo yanasemwa katika kuchinjwa siku ya ´Iyd. Kile kinachochinjwa na yule mwenye kuhiji anasema:
الله أكبر
“Allaah ni mkubwa.”
Vichinjwa vyenginevyo aseme:
باسم الله
“Kwa jina la Allaah.”
[1] 06:162
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
- Imechapishwa: 15/09/2019
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)