Kusinzia hakuchengui wudhuu´ tofauti na kulala

Swali: Kuna mwanamke amejitwahirisha kisha akalala ndani ya gari akiwa njiani kuelekea Makkah ambapo akatufu bila kutawadha. Akabaki akiwa mwenye kufanya Tamattu´ mpaka hajj na akamaliza hajj yake na ikamalizika Ihraam yake. Kipi kinachomlazimu?

Jibu: Hapana neno ikiwa kulala kulikomjia ni kwa njia ya kusinzia. Kusinzia hakuchengui wudhuu´. Lakini ikiwa ni usingizi mzito wa aina ambayo unachengua wudhuu´, basi hukumu yake ni kama ambaye hakutufu Ka´bah. Kwa hivyo atakuwa Qaarinah. Twawaaf-ul-Ifaadhwah na Sa´y ya Ifaadhwah inatosheleza na Twawaaf ya ´Umrah na Sa´y yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/142)
  • Imechapishwa: 20/08/2021