Kusimama wakati kunapopitishwa jeneza

Swali: Je, inachukiza kusimama kwa ajili ya jeneza linapokuja?

Jibu: Hapana. Inapendeza kusimama kwa ajili ya jeneza linapokaribia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mkiona jeneza simameni.”

Sunnah ni kusimama kwa ajili yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza katika Hadiyth kwamba:

”Tumekuja kusimama kwa ajili ya Malaika.”

Imekuja katika tamko jengine:

”Hakika mauti yanatia khofu.”

Imekuja katika tamko jengine:

”Je, si ni nafsi?”

Basi Sunnah ni kusimama kwa ajili ya jeneza, lakini si wajibu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisimama na pia aliketi (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aliposimama na kuketi inaonyesha kuwa kusimama si wajibu. Atakayesimama anapoiona jeneza inakuja mpaka ipite mbele yake, hilo ndilo bora. Akikaa bila kusimama basi hapana neno na hapana ubaya. Lakini mwenye kusindikiza jeneza, huyo anatakiwa kusimama mpaka iwekwe chini, kwa kuwa anayesindikiza jeneza anatembea pamoja nayo. Sunnah kwake ni kubaki amesimama mpaka iwekwe ardhini kutoka juu ya vichwa vya wanaume au kutoka kwenye gari ikiwa inasafirishwa kwa gari, mpaka iwekwe ardhini.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1019/حكم-القيام-للجنازة
  • Imechapishwa: 07/01/2026