Kusilimu kwa mwanaume ndio mahari yako

Swali: Vipi kuhusu yale yaliyotangaa kwa Umm Sulaym kufanya kusilimu kwa Abu Twalhah ndio mahari yake?

Jibu: Hivi ndivo wanavoona baadhi ya wanazuoni kwamba mwanamke kufanya kusilimu kwa mwanaume au kumfunza Qur-aan ndio mahari yake na kwamba hapana vibaya kwa hilo. Hata hivyo Aayah ilishuka baada ya hapo. Aayah ya an-Nisaa´ ambayo ni ya al-Madiynah:

أَن تَبْتَغُوا بِأَمْوَالِكُم

”… mtafute [kuwaoa] kwa mali zenu… ”[1]

inafahamisha kuwa ni lazima kuwepo mali. Kuna uwezekano vilevile kisa cha Umm Sulaym ni kabla ya kushuka kwa Aayah. Ni lazima kufaradhisha pesa ingawa zitakuwa kidogo:

أَن تَبْتَغُوا بِأَمْوَالِكُم

”… mtafute [kuwaoa] kwa mali zenu… ”

[1] 04:24

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23840/حكم-جعل-اسلام-الرجل-او-تعليم-القران-مهرا
  • Imechapishwa: 18/05/2024