Swali: Ni ipi hukumu ya kusikiliza Anaashiyd zenye kuambatana na dufu zikiimbwa kwa sauti za wanaume?

Jibu: Hili halifai. Dufu inaruhusiwa kwa wanawake katika harusi, na pia kwa wasichana wadogo katika siku za ´Iyd. Hivo ndivo ilivyokuwa wajakazi wakiimba wakati wa ´Iyd katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). kuhusu wanaume, hilo halifai.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
  • Imechapishwa: 16/09/2026