Swali: Kuna mswaliji mmoja kila anapomaliza kuswali Fajr na kumdhukuru Allaah, anasujudu Sujuud moja kwa ajili ya kumshukuru Allaah kabla ya kutoka nje…

Jibu: Hii ni Bid´ah. Sujuud inafanywa wakati wa kufanywa upya neema au kusalimika na janga. Ama kusujudu kila wakati na kusema kuwa ni kwa ajili ya kumshukuru Allaah si sahihi. Swalah ni kitu cha kawaida na sio kitu kilichofanyika upya. Ametekeleza faradhi yake. Mwambie asiendelee na jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (29)
  • Imechapishwa: 11/02/2022