Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa Rifaa´ah al-Juhaniy 3

70 – Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: al-´Abbaas bin Muhammad bin Haatim ametuhadithia: Mu´aadh bin Haani’ al-Yashkuriy ametuhadithia: Harb bin Shaddaad ametuhadithia: Yahyaa bin Abiy Kathiyr ametuhadithia: Hilaal bin Abiy Maymuunah amenihadithia: ´Atwaa’ bin Yasaar amenihadithia: Rifaa´ah bin ´Araabah al-Juhaniy amenihadithia:

“Siku moja tulikuwa nje pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)… Kisha akasema: “Kunapopita theluthi ya usiku, au nusu ya usiku, basi hushuka Allaah (´Azza wa Jall) katika mbingu ya chini na anasema mpaka kunaingia alfajiri: “Simuulizi yeyote juu ya waja Wangu zaidi yangu Mwenyewe. Ni nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe? Ni nani mwenye kuniomba nimuitikie? Ni nani mwenye kuniomba nimpe?”

Pia Abaan bin Yaziyd al-´Attwaar ameipokea kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 146-148
  • Imechapishwa: 29/04/2020