18-  Ahmad bin Muhammad bin Ziyaad al-Qattwaan ametuhadithia na Ibn Saa´id alisomewa na mimi huku nasikiliza: Ahmad bin Mansuur amekuhadithieni: ´Abdul-Wahhaab bin ´Atwaa’ ametuhadithia: Muhammad bin ´Amr ametuhadithia, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) anashuka kila usiku katika mbingu ya dunia kwenye nusu ya usiku au theluthi ya mwisho na anasema mpaka alfajiri inaingia: “Ni nani aniombaye nimuitikie? Ni nani aniombae nimpe? Ni nani aniombae maghfirah nimghufurie?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 104
  • Imechapishwa: 17/01/2018