40 – Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Ahmad bin Yuusuf as-Sulamiy ametuhadithia: Hajjaaj ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa ´Ubaydullaah bin ´Umar, kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Sa´iyd al-Maqbariy, kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allâhu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kunapopita theluthi ya usiku au nusu yake basi hushuka Allaah (´Azza wa Jall) katika mbingu ya dunia na kusema: ”Je, kuna mwenye kuomba nimpe? Je, kuna mwenye kuomba nimpe? Je, kuna mwenye kuomba msamaha nimsamehe?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 124
  • Imechapishwa: 21/01/2020