31- Abu Muhammad bin Swaa´id alisomewa na mimi nasikiliza: Muhammad bin ´Aliy bin Zanjuuyah amekuhadithieni: ´Aliy bin Muhammad al-Baswriy alisomewa huku nikisikiliza: Haashim bin Yuunus amekuhadithieni: Abu Swaalih ´Abdullaah bin Swaalih ametuhadithia: al-Layth bin Sa´d amenihadithia, kutoka kwa Yuunus, kutoka kwa Ibn Shihaab: Abu Salamah na Abu ´Abdillaah al-Agharr amenikhabarisha kwamba wamemsikia Abu Hurayrah akisema: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola wetu (´Azza wa Jall) hushuka pindi kunapobaki theluthi ya mwisho ya usiku katika mbingu ya dunia na husema: “Ni nani mwenye kuniomba nimpe? Ni nani mwenye kuniomba msamaha?”

Shu´ayb bin Abiy Hamzah vilevile ameipokea kupitia kwa az-Zuhriy.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 115
  • Imechapishwa: 15/01/2020