Swali: Nimesoma makala ambayo mwandishi wake ameipa jina “Lutwfu Allaahi bil-Khalq”1 ambapo mwandishi wake amekariri na kusema kuwa Ahl-us-Sunnah ndio kundi lililo karibu na haki. Ameyanasibisha maneno haya kwako. Tumetatizwa na hilo. Je, hili ni sahihi?

Jibu: Ahl-us-Sunnah ndio watu wa haki na si kwamba ndio watu walioko karibu na haki. Ahl-us-Sunnah ndio watu wa haki. Ikiwa ana ushahidi kuwa nilisema haya aniletee tuone. Ama kumnasibishia tu mtu kitu bila ya dalili haijuzu. Ahl-us-Sunnah ndio watu wa haki na si kusema kuwa ndio watu walio karibu na haki.

[1] Tazama https://sh-yahia.net/show_art_15.html

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (28) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-5-9.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020