Swali: Baadhi ya al-Ikhwaan al-Muslimuun wanataka ubainishe kuwa ulinganizi wao ni wa Kiislamu na sahihi na kwamba jukumu lao sio kuchokoza, kutafuta makosa au kuwajeruhi watu na mamlaka. Wanasema kuwa wao wako mbali kabisa na mambo hayo. Wanasema kuwa mambo kama hayo yanazuia dhamira yao ya kisiasa na kwamba linasababisha mipasuko, kwani jukumu lao ni kuleta umoja na kutofarikisha, kujenga na kutobomoa, kushirikiana katika yale ambayo tumeafikina na kupeana udhuru katika yale ambayo tumetofautiana. Je, haya ni sawa?
Jibu: Sehemu ya mwisho inapinga sehemu yake ya mwisho. Wanasema kuwa wao hawawajeruhi watu. Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia swahiba yake:
إِنَّكَ لَغَوِيٌّ مُّبِينٌ
”Hakika wewe ni mpotofu wa wazi.”[1]
Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Abu Dharr:
“Hakika wewe ni mtu una chembechembe za kipindi kabla ya kuja Uislamu.”[2]
Alimwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anh):
“Je, wewe ni mfitini mkubwa, ee Mu´aadh?”[3]
Alisema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati bwana mmoja alipotaka kuingia ndani na kuzungumza naye:
“Mwache aingie. Ndugu mbaya aliyoje!”[4]
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tena:
“Sidhani kuwa fulani na fulani wanatambua katika dini yetu chochote.”[5]
Alimkubalia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Hindi kumweleza Abu Sufyaan (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kuwa ni mwanaume mchoyo[6].
Yote haya ni mfano wa kujeruhi, jambo ambalo halikubaliwi na ufahamu wao wenye maradhi. Si maimamu wa kujeruhi na kusifu peke yao, bali wanazuoni wote kwa jumla, wamekubaliana juu ya kufaa kujeruhi na kusifu.
Ukweli ni kwamba ulingano wa al-Ikhwaan al-Muslimuun ni kukusanya tu watu. Humo yumo Suufiyyah, Shiy´ah, Sunnah, mtenda dhambi, watu wa dunia na kila mtu. Jambo limekuwa baya zaidi pale walipowaingiza pia wakuu wa makabila wanaohukumu kwa kanuni na desturi kabla ya kuja Uislamu waliojiunga nao. Kuna mabalaa mengi mno.
Tunasema namna hii: ni wajibu kwetu na kwao kutojadili na watu wa batili. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَلَا تُجَادِلْ عَنِ الَّذِينَ يَخْتَانُونَ أَنفُسَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ خَوَّانًا أَثِيمًا
”Wala usiwatetee wale wanaokhini nafsi zao. Hakika Allaah Hampendi aliye mwingi wa kukhini na kutenda dhambi.”[7]
Kusema kwamba ulinganizi wao unakusanya na haufarikishi ni dalili kubwa inayoonyesha kuwa inahusiana na kukusanya watu peke yake. Lakini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Muhammad ni mwenye kufarikisha kati ya watu.”[8]
Bi maana mtoto wa Kiislamu na baba yake akawa kafiri, mwanamke wa Kiislamu na mume wake akawa kafiri na kinyume chake. Ndugu akiwa muislamu na mwingine akawa kafiri, wanatengana. Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa ni mwenye kutenganisha kati ya watu. Sijui kama watu hawa wanaelewa kile wanachosema.
Baya zaidi kuliko haya ni pale wanaposema kuwa wanashirikiana katika yale wanayoafikiana na kupeana udhuru katika yale wanayotofautiana. Tangu hapo zamani nilikwambieni kuwa myageuze maneno hayo yawe hivi:
“Tunashirikiana katika yale tunayofikiana na kuamrishana mema, kukatazana maovu, tunanasihiana katika yale tunayotofautiana.”
Mfumo wao ni kwamba muda uko pamoja nasi, basi fanya Bid´ah uwezavyo; bado wewe ni ndugu yetu. Hivo ndivo wanavokuwa Hizbiyyuun. Na ukiwa hauko pamoja nasi, wanakuona kuwa ni muharibifu na mfisadi ambaye ni khatari katika jamii. Tangu hapo zamani mimi niliwaambia al-Ikhwaan al-Muslimuun kuukagua mfumo wao. Tangu hapo kitambo walipotoka mitaani wakiandamana dhidi ya Saddaam na dhidi ya katiba, niliwaambia kuwa mfumo kama huo hauwalei wanaume. Ni lazima mrudi kuukagua mfumo wenu. Vinginevyo mtabaki kuwa kama mpira unaopigwa kutoka kila upande. Tazama historia yao Misri, Syria na Sudan – ni historia nyeusi iliyoathiri vibaya Uislamu na ulinganizi.
[1] 28:18
[2] al-Bukhaariy (30) na Muslim (1661).
[3] Ahmad (3/299), al-Bukhaariy (705) na Muslim (465).
[4] Ahmad (6/38), al-Bukhaariy (6032) na Muslim (2591).
[5] al-Bukhaariy (6067).
[6] Muslim (1714).
[7] 4:107
[8] al-Bukhaariy (7281).
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 333-335
- Imechapishwa: 06/07/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket