Swali: Maneno ya Ibn ´Abbaas:

“Ataoga na kuswali ijapo ni kwa saa.”

Ina maana kwamba hata kama atasafika saa limoja tu?

Jibu: Pale atakapoona kusafika kwa kawaida.

Swali: Ijapo ni kwa saa limoja?

Jibu: Hata kama. Akiona kuwa amesafika ataoga na kuswali. Hayo ndio makusudio.

Swali: Damu ikirudi?

Jibu: Atakaa ikiwa imetokea katika ule muda wake. Kisha ikiwa sio katika ada yake ni damu ya ugonjwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23557/معنى-تغتسل-وتصلي-ولو-ساعة-للحاىض
  • Imechapishwa: 10/02/2024