Kurudi kuishi shambani baada ya kuhajiri

Swali: Mtu anayerejea katika maisha ya shambani baada ya kuhajiri?

Jibu: Dhahiri ni makatazo, kwa sababu Allaah alipombebesha neema ya kuhajiri basi harudi kuwa mtu wa shambani isipokuwa kwa haja. Ikiharibika hali ya miji, basi atatoka kwenda shambani ili kuhifadhi dini yake, kama ilivyokuja katika Hadiyth Swahiyh kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa kuhusu watu bora ambapo akasema:

”Muumini anayepambana jihaad katika njia ya Allaah… ” kisha akasema: ”Muumini aliye katika njia za milimani akimwabudu Allaah na kuwaacha watu na shari yao.”

ar-Raajihiy: Je, kurudi maisha ya shambani ni dhambi kubwa bila haja?

Ibn Baaz: Kurejea maisha ya shambani baada ya kuhajiri, ndio, ni katika madhambi makubwa, ndio.

Mwanafunzi: Hukumu ya yule anayerejea maisha ya shambani baada ya kuhajiri bado ipo mpaka sasa?

Ibn Baaz: Ndio, isipokuwa kutokana na sababu. Ikiwa jamii imeharibika na akatoka katika jamii ili kuhifadhi dini yake.

Mwanafunzi: Kwa maana ya kwamba haipelekei kutokuwepo kuhajiri?

Ibn Baaz: Ikiwa ametoka kwa ajili ya kuhifadhi dini yake, kwa sababu jamii ya mijini imebadilika, inafaa kwake kufanya hivyo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31640/ما-حكم-من-يرتد-اعرابيا-بعد-الهجرة
  • Imechapishwa: 21/12/2025