Kurefusha du´aa ya kumuombea maiti baada ya kumzika

Swali: Nilishiriki katika kulisindikiza jeneza katika katika moja ya miji ya Qaswiym. Baada ya kumalizika kuzika wakanyunyizia maji na waliokuja kuzika wakasimama kwa ajili ya kumuombea du´aa maiti lakini hata hivyo wakasimama kwa kurefusha sana na wakasema kuwa kitendo hichi ndio Sunnah. Imepokelewa kwamba kusimama ni sawa na kumchinja ngamia na kumgawa. Ni upi usahihi wa hilo?

Jibu: Watu wanapomalizika kumzika maiti Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alichokuwa anafanya pindi kunapomalizwa kumzika maiti anasimama karibu naye na anasema:

“Muombeeni msamaha ndugu yenu. Kwani hakika hivi sasa anahojiwa.”

Hakuwa anaomba pamoja nao du´aa ya kwa pamoja. Bali kila mmoja anaomba kivyake. Vilevile hakuwa anarefusha kisimamo. Miongoni mwa mazowea ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwamba anapoomba basi huomba mara tatu. Kujengea juu ya hili inatosha kusema:

اللهم اغفر له، اللهم اغفر له، اللهم اغفر له، اللهم ثبته، اللهم ثبته، اللهم ثبته

“Ee Allaah! Msamehe! Ee Allaah! Msamehe! Ee Allaah! Msamehe! Ee Allaah! Mthibitishe! Ee Allaah! Mthibitishe! Ee Allaah! Mthibitishe!”

Baada ya hapo unaondoka nazo.

Kuhusu kukaa au kusimama kwa kiasi cha kumchinja ngamia na kuigawa nyama yake ni jambo limesemwa na ´Amr bin al-Aasw (Radhiya Allaahu ´anh) wakati alipoacha wasia. Lakini hata hivyo sio katika mwongozo wenye kuenea wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah wengine. Ni jambo aliacha anausia kutokana na Ijtihaad yake (Radhiya Allaahu ´anh) na akasema:

“Mpaka wataporudi wajumbe wa Mola wangu.”

Akimaanisha Malaika wanaokuja kuhoji. Vile ninavyoona ni kwamba watu wanatakiwa kutendea kazi yale ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiyafanya. Kuhusu wasia wa ´Amr bin al-Aasw (Radhiya Allaahu ´anh) ni Ijtihaad yake. Sunnah imesimama juu ya kutokufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (67) http://binothaimeen.net/content/1517
  • Imechapishwa: 12/02/2020