Kurauka kwa kula tende 7 ni kwa tende za Madiynah peke yake?

Swali: Ni kuhusu tende za Madiynah peke yake?

Jibu: Huo ndio udhahiri wa Hadiyth. Hata hivyo kuna matarajio juu tende aina zingine. Kwa sababu baadhi ya mapokezi yanasema:

“Yule mwenye kupambaukiwa na akala tende saba basi hatodhurika siku hiyo kwa sumu wala uchawi.”

Kwa hivyo kunaingia aina zote za tende. Hata hivyo tamko linalosema:

“Yule mwenye kupambaukiwa na akala tende saba basi hatodhurika siku hiyo kwa sumu wala uchawi.”[1]

“Yule mwenye kupambaukiwa na akala tende saba za ´Ajwah za Madiynah… ”

yanafahamisha kuwa ni tende maalum na kwamba aina hizi za tende ndio bora kuliko zingine.

[1] al-Bukhaariy (5445) na Muslim (2047).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23991/هل-التصبح-بسبع-تمرات-خاص-بتمر-المدينة
  • Imechapishwa: 09/08/2024