Kupitisha maji kati ya vidole vya miguuni na mkononi

Swali: Je, kupitisha maji kati ya vidole ni jambo la lazima?

Jibu: Ndio.

Swali: Imetajwa kwamba ni katika mambo yanayopendekezwa?

Jibu: Kupitisha maji kati ya vidole ni amri ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ikiwa mtu ana khofu kwamba maji hayatofika, basi ni lazima kupitisha maji. Lakini kama mtu ana yakini kuwa maji yatafika, basi kupitisha maji kunakuwa ni jambo linalopendekezwa. Maana ya kupitisha maji kati ya vidole ni kwamba inapendekezwa ikiwa maji yanafika, lakini kama maji hayatofika, basi ni wajibu kupitisha.

Swali: Hapa imesemwa kwa ujumla?

Jibu: Hayo ni makosa. Lazima kuwe na ufafanuzi, kwa sababu wakati mwingine vidole huwa vimebanana au huwa na kitu katikati yake. Kwa hivyo katika hali hiyo ni lazima kupitisha maji khaswa kati ya vidole vya miguu. Wakati mwingine kati ya vidole vya mikono, huenda kukawa na kitu baina yake. Lakini ikiwa ni safi hakuna tatizo, basi inakuwa ni jambo linalopendekezwa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31513/ما-حكم-تخليل-الاصابع-في-الوضوء
  • Imechapishwa: 30/10/2025