Kupitiliza juu ya midoli yenye picha kwa hoja eti ya kisa cha ´Aaishah

Swali: Picha zinazowekwa kwa ajili ya watoto baadhi ya watu wameenda mbali zaidi katika jambo hili na sasa, ee Shaykh, kuna hata filamu zenye picha?

Jibu: Kilicho na tahadhari zaidi ni kuziteketeza. Baadhi ya wanazuoni wamejizusha kwa sababu ni vitu vinavyodharauliwa kwa watoto. Wanatoa hoja kwa kisa cha ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambapo alisema kumwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomtajia kuhusu midoli na wasichana zake:

“Kwangu kuna mdoli wa mfano wa farasi mwenye mabawa.” Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akacheka akasema: “Farasi mwenye mabawa?!”

Wamejengea hoja kwa hilo. Lakini hili linachukuliwa kuwa lilikuwa kabla ya kukatazwa na kabla ya kuzuiwa, au picha hizo ni zile zinazotengenezwa kwa mikono ya watu ambazo si halisi. Watu wengine huchezea tu, husuka vipande vya nguo au pamba na kuunda, lakini si picha halisi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28970/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%88%D8%B1-%D9%88%D8%A7%D9%84%D8%A7%D9%81%D9%84%D8%A7%D9%85%C2%A0%D8%A7%D9%84%D8%AA%D9%8A-%D8%AA%D8%AC%D8%B9%D9%84-%D9%84%D9%84%D8%A7%D8%B7%D9%81%D8%A7%D9%84
  • Imechapishwa: 15/05/2025