Kupinga kuwa mayahudi na manaswara wa leo sio Ahl-ul-Kitaab

Swali: Mwenye kusema mayahudi na manaswara wa leo sio Ahl-ul-Kitaab kama walivyokuwa katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kujengea juu ya hilo haijuzu kuoa kutoka kwao. Je, maoni yake ni sahihi?

Jibu: Haya ni maneno batili. Allaah kawaita kuwa ni Ahl-ul-Kitaab na akahalalisha kuoa wanawake wao ambao ni watwaharifu na zinaa, bi maana Muhswanaat:

وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ

“… [pia mmehalalishiwa kuwaoa] muhswanaatu miongoni mwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu.” (05:05)

Muhswanaat ni wepi? Ni wale waliotakasika na zinaa, ni mamoja ikiwa ni zinaa ya hadharani au ya kujificha:

غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ

”… bila ya kufanya uhasharati wala kuchukua hawara.” (05:05)

Inajuzu kuoa kwao. Allaah Amehalalisha hili mpaka siku ya Qiyaamah. Wewe unampinga Allaah na kusema “Hapana, wao sio Ahl-ul-Kitaab”? Ni nani anayesema hivi? Tangu wakati Qur-aan ilipokuwa inateremka walikuwa wanasema Allaah ni utatu na al-Masiyh ni mwana wa Allaah, pamoja na haya Allaah amewaita kuwa ni Ahl-ul-Kitaab.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fth-mjd-17051435.mp3
  • Imechapishwa: 20/09/2020