Swali: Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Si vinginevyo jambo la kupiga mokofi ni kwa wanawake.”

ni Hadiyth? Ni upi usahihi wake?

Jibu: Hadiyth hii imethibiti katika al-Bukhaariy na ndani yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mna nini nyinyi pindi mnapozindua jambo mnapiga makofi? Si vinginevyo jambo la kupiga mokofi ni kwa wanawake.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (09) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191370#219699
  • Imechapishwa: 16/03/2019