Kupiga hatua kadhaa ndani ya swalah kuziba uwazi kwenye safu

Swali: Kugeukageuka kualini na kushotoni ndani ya swalah wakati kunapokimiwa swalah na alikuwa anaswali swalah ya kujitolea?

Jibu: Haidhuru. Ni sawa pia akitembea kwa ajili ya kuziba uwazi kushotoni mwake. Hapana vibaya akiwa upande wa kuliani au kushotoni mwa safu na akatembea kwa ajili ya kuzipa uwazi. Kufanya hivo kumesuniwa kwa ajili ya manufaa.

Swali: Hata kama atatikisika sana?

Jibu: Hata kama.

Swali: Wakati mwingine anahitaji kuvuka safu mbili au safu tatu?

Jibu: Haidhuru, kwa sababu kufanya hivo ni kwa ajili ya manufaa ya swalah anataka kuziba uwazi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24819/حكم-الخطوات-الى-اليمين-والشمال-في-الصلاة
  • Imechapishwa: 14/12/2024