Swali: Tumeamrishwa kuunga kizazi, lakini kuna tatizo katika jambo hili. Tunapowatembelea jamaa zetu tunalazimika kuwapa mkono wanawake ambao inafaa kwetu kuwaoa. Je, inafaa kupeana mkono na mke wa ami akiwa ni mzee?
Jibu: Umeamrishwa kuwaunga ndugu na umekatazwa kupeana mkono na wanawake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mimi sipeani mkono na wanawake.”[1]
´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:
“Naapa kwa Allaah Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwahi hata siku moja kugusa mkono na mwanamke.”[2]
Ma´qal bin Yasaar amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mtu kuchomwa sindano ya chuma kichwani mwake ni bora kwake kuliko kumgusa mwanamke asiyekuwa halali kwake.”[3]
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
قُل لِّلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا مِنْ أَبْصَارِهِمْ وَيَحْفَظُوا فُرُوجَهُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَزْكَىٰ لَهُمْ
”Waambie waumini wanaume wainamishe macho yao na wahifadhi tupu zao. Hivyo ni utakaso zaidi kwao.”[4]
Ni vipi utapeana mkono kisha udai kuwa unayashusha macho yako? Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwanadamu ameandikiwa sehemu ya uzinzi na haiepukiki. Uzinzi wa macho ni kule kuangalia. Uzinzi wa masikio ni kule kusikiliza. Uzinzi wa ulimi ni kule kuongea. Uzinzi wa mkono ni kule kugusa. Uzinzi wa miguu ni kule kutembea. Nafsi inatamani na kutaka na tupu ndio ima inasayadikisha au kuyakadhibisha hayo.”[5]
Kwa maana nyingine ni kwamba unatakiwa kuwaunga jamaa zako na kuwatembelea ndugu zako na usipeane mkono na wanawake. Unalazimika kuwafunza dini ya Uislamu. Vivyo hivyo kuhusu mwanamke mtumzima; haijuzu kwako kupeana naye mkono. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mimi sipeani mkono na wanawake.”
Hakumbagua mwanamke yeyote. Ni sahihi kwamba inafaa kukaa na kuzungumza na mwanamke mtumzima, lakini usiketi naye chemba. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَالْقَوَاعِدُ مِنَ النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا يَرْجُونَ نِكَاحًا فَلَيْسَ عَلَيْهِنَّ جُنَاحٌ أَن يَضَعْنَ ثِيَابَهُنَّ غَيْرَ مُتَبَرِّجَاتٍ بِزِينَةٍ
”Wanawake wazee waliokatika hedhi ambao hawataraji kuolewa, hakuna ubaya juu yao kupunguza baadhi ya nguo zao bila ya kudhihirisha mapambo yao.”[6]
[1] an-Nasaa’iy (4192). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan an-Nasaa’iy” (4192).
[2] Muslim (1866).
[3] ar–Rawaayaaniy (2/227). Cheni ya wapokezi ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah” (226).
[4] 24:30
[5] al-Bukhaariy (6243) na Muslim (2657).
[6] 24:60
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 412-413
- Imechapishwa: 08/07/2025

Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 412-413
Imechapishwa: 08/07/2025
https://firqatunnajia.com/kupeana-mkono-na-mke-wake-ami-mzee/