Kupeana mikono na dada yake ndugu yangu upande wa baba

Swali: Ikiwa kuna ndugu wa upande wa baba ambaye ana dada wa kunyonya – Je, inajuzu kwangu kumsalimia kwa kushikana mikono?

Jibu: Ikiwa dada huyo wa kunyonya alinyonyeshwa na mke wa baba yako, basi huyo ni dada yako na ni dada yake yeye pia. Hivyo anakuwa ni dada kwako kupitia baba kwa upande wa kunyonya na inahesabika kama undugu wa kuchangia ziwa. Ama ikiwa ndugu yako wa upande wa baba alinyonyeshwa na mwanamke mwingine, asiye mke wa baba yako, basi mwanamke huyo anakuwa ni mama yake wa kunyonya peke yake, wala si mama yako.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1804/حكم-مصافحة-اخت-الاخ-من-الاب-من-الرضاعة
  • Imechapishwa: 27/12/2025