Kupangusa juu ya soksi pea nyingine ambayo aliivaa baada ya kuchenguka wudhuu´

Swali: Nilivaa soksi baada ya wudhuu´ na kukamilika kwa twahara. Kisha baada ya muda mmoja au miwili, nikavaa juu yake soksi nyingine kwa ajili ya kujikinga na baridi, hali nikiwa nimechenguka wudhuu´. Je, inajuzu kupangusa juu ya soksi ya pili?

Jibu: Mwenye kuuliza anasema kuwa alivaa soksi akiwa na twahara. Kisha baada ya kupita muda mmoja au miwili, akavaa juu yake soksi nyingine kwa ajili ya joto, hali yake ikiwa si mwenye twahara. Jibu ni kwamba haijuzu kufuta juu ya soksi ya pili. Haifai, kwa sababu amevaa soksi hiyo ya pili akiwa hana twahara. Lakini lau angeivaa akiwa na twahara, kwa maana kwamba akatawadha, kisha akapangusa juu ya soksi ya kwanza, halafu akavaa soksi ya pili akiwa bado katika twahara hiyo, basi ingejuzu kupangusa juu yake kwa sababu ameivaa akiwa na twahara. Lakini akivaa soksi hiyo ya pili baada ya kuchenguka wudhuu´, basi atakuwa ameivaa bila twahara na hivyo hapaswi kupangusa juu yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1124/مسالة-في-المسح-على-الجوارب
  • Imechapishwa: 30/01/2026