Kupanga swawm ya sunnah na vijana wengine

Swali: Sisi ni kikosi cha vijana wenye dini ambao tunafunga kila alkhamisi na tunafuturu nyumbani kwa mmoja kati yetu. Unasemaje juu ya jambo hilo?

Jibu: Ikiwa katika kufanya hivo hakuna kumlazimisha yeyote, basi mtu anaweza kusema kuwa kitendo hicho hakina neno. Lakini mimi napendelea kila mmoja afunge kivyake na afuturu kivyake, afunge pale anapotaka na aache kufunga pale anapotaka. Hii ndio Sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fath-ur-Rahiym al-Waduud, uk. 259
  • Imechapishwa: 20/06/2020