Kuozeshwa na walii mtenda madhambi

Swali: Vipi ikiwa walii wa mwanamke ni mtenda maasi?

Jibu: Haijalishi kitu. Sahihi ni kwamba atamuozesha ijapokuwa sio mwadilifu. Mwanamke asijiozeshe mwenyewe. Hata hivyo akipatikana walii mwadilifu basi yeye ana haki zaidi kuliko mwingine. Sahihi ni kwamba hakushurutishwi uadilifu katika uwalii, kwa sababu ghera ipo. Kwa hivyo aozeshwe na walii wake; baba yake au jamaa wa karibu zaidi na zaidi. Haijalishi kitu ikiwa atakuwa na mapungufu katika uadilifu. Asijiozeshe mwenyewe.

Swali: Vipi ikiwa Bid´ah zake ni za kishirki?

Jibu: Hapana, kafiri hana uwalii wowote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23834/هل-تزوج-نفسها-من-كان-وليها-عاصيا
  • Imechapishwa: 08/05/2024