Swali: Katika TV kunaonyeshwa mieleka mbele ya wanawake na viungo visivyotakiwa kuonekana kwa wale wafanya mieleka vinaonekana waziwazi mbele yao. Unasemaje juu ya jambo hilo?
Jibu: Haijuzu kuonyesha kinachobainisha viungo visivyotakiwa kuonekana. Ni mamoja mchezo huo ni wa mweleka au mashindano kama mfano wa mchezo wa mpira na nyenginezo. Kila mchezo unaonyesha viungo visivyotakiwa kuonekana au unapoteza swalah haifai kuuhudhuria. Lakini hakuna neno ikiwa vinafunikwa viungo visivyotakiwa kuonekana, hakufanywi mambo ya haramu na wala swalah hazipotezwi. Ikiwa katika mieleka hiyo viungo visivyotakiwa kuonekana vinaonekana, basi itakuwa ni haramu kwa wanamme na wanawake wote. Vivyo hivyo kuhusu mchezo wa mpira ikiwa viungo visivyotakiwa kuonekana vitabaki wazi na mapaja basi itakuwa ni haramu jambo hilo kwa wote. Isitoshe hilo likipelekea kuzipoteza swalah ndani ya wakati wake au swalah kwa mkusanyiko basi itakuwa ni haramu kwa wote. Tunamuomba Allaah uongofu.
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaad-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4844/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B8%D9%87%D9%88%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D8%B9%D9%88%D8%B1%D8%A9-%D9%81%D9%8A-%D8%B1%D9%8A%D8%A7%D8%B6%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%B1%D8%AC%D8%A7%D9%84
- Imechapishwa: 23/11/2020
Swali: Katika TV kunaonyeshwa mieleka mbele ya wanawake na viungo visivyotakiwa kuonekana kwa wale wafanya mieleka vinaonekana waziwazi mbele yao. Unasemaje juu ya jambo hilo?
Jibu: Haijuzu kuonyesha kinachobainisha viungo visivyotakiwa kuonekana. Ni mamoja mchezo huo ni wa mweleka au mashindano kama mfano wa mchezo wa mpira na nyenginezo. Kila mchezo unaonyesha viungo visivyotakiwa kuonekana au unapoteza swalah haifai kuuhudhuria. Lakini hakuna neno ikiwa vinafunikwa viungo visivyotakiwa kuonekana, hakufanywi mambo ya haramu na wala swalah hazipotezwi. Ikiwa katika mieleka hiyo viungo visivyotakiwa kuonekana vinaonekana, basi itakuwa ni haramu kwa wanamme na wanawake wote. Vivyo hivyo kuhusu mchezo wa mpira ikiwa viungo visivyotakiwa kuonekana vitabaki wazi na mapaja basi itakuwa ni haramu jambo hilo kwa wote. Isitoshe hilo likipelekea kuzipoteza swalah ndani ya wakati wake au swalah kwa mkusanyiko basi itakuwa ni haramu kwa wote. Tunamuomba Allaah uongofu.
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaad-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4844/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B8%D9%87%D9%88%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D8%B9%D9%88%D8%B1%D8%A9-%D9%81%D9%8A-%D8%B1%D9%8A%D8%A7%D8%B6%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%B1%D8%AC%D8%A7%D9%84
Imechapishwa: 23/11/2020
https://firqatunnajia.com/kuonyesha-viungo-visivyotakiwa-kuonekana-wakati-wa-michezo/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)