Swali: Ni ipi hukumu ya mtu kuomba sifa miongoni mwa sifa za Allaah?

Jibu: Haijuzu kuomba sifa. Mtu anatakiwa kufanya Tawassul kwazo:

”Ee Allaah! Ninakuomba kwa kukupenda kwangu, najilinda kwa radhi Yako kutokana na ghadhabu Zako na kwa msamaha Wako kutokana na adhabu Yako.”

Mtu anafanya Tawassul kwazo. Haifai kuziomba:

”Ee jicho la Allaah, tufanyie kadhaa! Ee mkono wa Allaah, turuzuku! Ee maneno ya Allaah, tusaidie!”

Haifai. Bali mtu aseme:

”Ee Allaah! Ee Mwingi wa rehema! Ee Mwenye kurehemu!”

Anaombwa kwa majina Yake (Jalla wa ´Alaa). Sifa haziombwi kwa maafikiano ya waislamu. Hivo ndivo alivyosema Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah). Mtu anatakiwa kufanya Tawassul kwazo na kuomba ulinzi kwazo:

”Ee Allaah! Hakika mimi najilinda kwa radhi Yako kutokana na ghadhabu Zako na kwa msamaha Wako kutokana na adhabu Yako. Nakutaka msaada kwa rehema Yako, ee Mola wangu.”

Na mfano wa hayo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30980/هل-يجوز-دعاء-الصفة-من-صفات-الله
  • Imechapishwa: 19/09/2025