Kuomba du´aa dhidi ya aliyekufanyia uchawi

Swali: Nateseka na uchawi tokea miaka tatu ya nyuma. Sipati usingizi wala sihisi ladha ya chakula. Inajuzu kwangu kuomba du´aa dhidi ya yule aliyenifanyia uchawi?

Jibu: Hili halitatui tatizo. Kuomba du´aa dhidi yake hakuondoi uchawi ulionao. Ni juu yako kufanya Ruqyah ya Kishari´ah, matibabu mazuri na yenye manufaa. Allaah hakuteremsha ugonjwa isipokuwa ameteremsha pia dawa yake; mwenye kujua, ameijua na ambaye hakuijua, hakuijua. Ni juu yako kufanya matibabu ya Kishari´ah pamoja, kukithirisha kumdhukuru Allaah na kuomba du´aa. Dawa iko mikononi mwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (7) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–15041434.mp3
  • Imechapishwa: 24/12/2016